RAIS WA TALTA AFUNGA KIKAO KAZI CHA MAAFISA USAFIRI WA SERIKALI, AWASISITIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 12, 2025

RAIS WA TALTA AFUNGA KIKAO KAZI CHA MAAFISA USAFIRI WA SERIKALI, AWASISITIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO


Rais wa Chama cha Wataalam wa Lojistiki na Usafirishaji Tanzania (TALTA), Bw. Alphonce Mwingira, leo ameongoza hafla ya kufunga kikao kazi cha Maafisa Usafiri wa Serikali kilichofanyika Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Royal Village kuanzia tarehe 11 Mpaka tarehe 12 Agosti, 2025.

Akizungumza katika kikao hicho Bw. Mwingira amesema kumekuwa na changamoto zinazoikumba sekta hii ya usafirishaji na maafisa usafiri wa Serikali kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa bodi ya usajili ya wataalamu wa usafirishaji, kutokuwepo kwa idara na vitengo rasmi vinavyosimamia maafisa usafirishaji, pamoja na mifumo ya kidigitali ya kutumia vyombo vya moto

Aidha, amesema lengo limefikiwa na wameandaa mapendekezo kwa Serikali kuhusu namna bora ya kutatua mapungufu yaliyobainika huku kazi iliyobaki kwa uongozi wa TATLA ni utekelezaji wa maazimio ikiwemo kuhakikisha mapendekezo hayo yanawasilishwa Wizara ya Uchukuzi kufikia tarehe 19 agosti, 2025

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa TALTA, Bw. Josephat Msomi, ametoa wito kwa Serikali kuendelea kuwekeza kwenye mafunzo endelevu na kuongeza bajeti ya matengenezo ya vyombo vya usafiri, ili kuhakikisha huduma bora na salama zinapatikana kwa watumishi na wananchi.

Aidha kikao kazi ,kimetoa mapendekezo kwa Serikali kukamilisha zoezi la uanzishwaji wa bodi ya usajili wa Wataalam wa Lojistiki na Usafirishaji, uhuishwaji wa kada ya lojistiki na usafirishaji ili iwe huru na Wizara ya Uchukuzi kuhakikisha inaandaa semina, warsha na vikao kazi vya mara kwa mara ili wataalam wabadilishane uzoefu na kuboresha utendaji kazi pia TALTA kuhakikisha vikao kama hivi vinafanyika kila mwaka

Kikao kazi hicho kilikusanya Maafisa usafiri kutoka Wizara,Idara,Wakala na Halmashauri mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili changamoto,mbinu na mikakati ya kuboresha usimamizi usimamizi wa rasilimali za usafiri wa Serikali kwa tija na ufanisi.


No comments:

Post a Comment