Samia Scholarship Yawasha Ndoto za Vijana wa Kitanzania Katika Teknolojia ya Kisasa - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 31, 2025

Samia Scholarship Yawasha Ndoto za Vijana wa Kitanzania Katika Teknolojia ya Kisasa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahitimu 50 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 na kuchaguliwa kupata ufadhili wa Samia Scholarship Extended, kusomea programu za Akili Unde, Sayansi ya Data na Sayansi zingine Shirikishi katika vyuo vikuu mahiri duniani.

Na.Mwandishi Wetu.

WAHITIMU 50 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 wamechaguliwa kupata ufadhili wa Samia Scholarship Extended, kusomea programu za Akili Unde, Sayansi ya Data na Sayansi zingine Shirikishi katika vyuo vikuu mahiri duniani.

Taarifa hiyo imetolewa Agosti 31, 2025 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ambaye amesema kuwa wahitimu waliochaguliwa walitokana na ufaulu wao bora katika masomo ya PCM, PMC na PGM.

Prof. Nombo amesema kuwa wanafunzi hao watawekwa katika Kambi Maalumu ya Maarifa (Boot camp), ambako watapatiwa mafunzo ya kujenga misingi katika matumizi ya kompyuta, programu na uchambuzi wa mifumo, pamoja na kusaidiwa kufanya maombi ya udahili katika vyuo vya nje kwa kushirikiana.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yatatolewa na wataalamu wabobezi kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo kutoka sekta binafsi na diaspora, kwa kipindi cha miezi 10.

Aidha watapata fursa ya kufanya mitihani itakayowawezesha kupata vyeti vya kitaaluma mfano IBM, Certificate- Machine Lerning for for Data Science Projects, Certified Certificate in Cyber Security Standards na AWS Certified Cloud Practitioner vinavyotambulika kimataifa.

Ufadhili huu ni utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, toleo la 2023, inayolenga kutoa elimu inayozingatia ujuzi kulingana na soko la ajira na stadi za karne ya 21 ili kuchangia katika maendeleo ya Taifa na kimataifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahitimu 50 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 na kuchaguliwa kupata ufadhili wa Samia Scholarship Extended, kusomea programu za Akili Unde, Sayansi ya Data na Sayansi zingine Shirikishi katika vyuo vikuu mahiri duniani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahitimu 50 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 na kuchaguliwa kupata ufadhili wa Samia Scholarship Extended, kusomea programu za Akili Unde, Sayansi ya Data na Sayansi zingine Shirikishi katika vyuo vikuu mahiri duniani.

Wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo (hayupo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wahitimu 50 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwenye matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2025 na kuchaguliwa kupata ufadhili wa Samia Scholarship Extended, kusomea programu za Akili Unde, Sayansi ya Data na Sayansi zingine Shirikishi katika vyuo vikuu mahiri duniani.

No comments:

Post a Comment