
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzingatia ulinzi na usalama wao kwanza ,wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi haswa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
Akifungua mafunzo kwa waandishi wa Habari, huko katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani Chake chake Pemba, mkufunzi wa mafunzo hayo Mwandishi Maryam Nassor ambae amejengewa uwezo na Umoja wa vilabu vya waandishi wa Habari Tanzania ( UTPC) . na yeye kutakiwa kuipeleka elimu hiyo kwa waandishi wengine

Mkufunzi huyo, amesema kuwa, ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari unaanza na mwandishi mwenyeye , hivyo kuwataka waandishi hao kuwa makini wanapotimiza majukumu yao.
“ Waandishi wa Habari lazima Kujifunza kusoma mazingira kwa haraka (kama vile maandamano au machafuko) ili kubaki salama wakati munatimiza majukumu yenu”
Amesema kuwa, tafiti zinaonesha katika kipindi hichi waandishi wengi huingia matatizoni na wengine kupoteza maisha.
Aidha ameongeza kuwa, ni vyema waandishi wa Habari kutoa taarifa kwa watu wao wa karibu , wanapokwenda kwenye kazi hatarishi, ili kuepuka hatari zinazoweza kujitokeza endapo watapatwa na hatari wakiwa pekee yao
“ Ulinzi na Usalama wa mwandishi wa Habari huanza na mwandishi mwenyewe hivyo ni lazima kutambua mazingira tunayofanyia kazi na watu tunaofanya nao kazi, ili kujihakikishia Ulinzi na Usalama wakati tunatimiza majukumu yetu” amesema .
Aidha amewataka waandishi wa Habari Kujua namna ya kushughulikia msongo wa mawazo baada ya kazi (trauma) na kupata mud awa kupumzika.
Mkufunzi huyo, amewaasa Waandishi wa habari kupata elimu ya saikolojia kwa sababu taaluma yao inawahusisha moja kwa moja na mazingira yenye changamoto nyingi za kiakili, kihisia, na kijamii.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mafuzo hayo, Fatma Hamad mwandishi wa blog ya Pemba ya leo na Is’haka Mohamed wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha usalama wao sehemu za kazi.
Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo Salum Hamad, amesema mafunzo hayo yamemuongezea uwelewa mkubwa wa kujua mipaka yake kama mwandishi katika kutekeleza majukumu yake
Mafunzo hayo, ya ulinzi na usalama wa kimwili, kimtandao na kisaikolojia yametolewa kwa baadhi ya waandishi wa Habari wa klabu ya waandishi wa Habari ya Pemba (PPC).
No comments:
Post a Comment