
Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete, amezindua Mfumo wa Kidijitali wa usimamizi wa mashauri ya usuluhishi na uamuzi unaotambulika kama "Online Case Management System" (OCMS) Leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mifumo ya kieletroniki na miongozo ya ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, amesema mfumo huu utaondoa adha na gharama za wadau kusafiri umbali mrefu kufuata haki zao.

Aidha, ameongeza kuwa mfumo huu ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali katika kuboresha huduma za haki-kazi nchini.
"Ikumbukwe, katika siku ya Wafanyakazi Duniani tarehe 01/05/2025 iliyofanyika mkoani Singida, Mhe. Rais aliujulisha umma kuhusu suluhisho la changamoto hiyo kwa serikali kuja na mfumo huu ambao utaboresha ufanisi wa CMA kutatua migogoro kwa wakati" amesema.
Mfumo huu wa usimamizi wa mashauri ya Usuluhishi na Uamuzi kidijitali utamuwezesha mwananchi kusajili mgogoro akiwa mahali popote kwa kutumia kifaa chenye intaneti kama vile simu janja, au kompyuta,kwa urahisi bila kufika ofisi ya Tume.
Mbali na OCMS, Mhe. Kikwete pia mezindua Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Soko la Ajira wa Mwaka 2025, pamoja na miongozo ifuatayo; Mwongozo wa Majadiliano Baina ya Serikali, Vyama vya Wafanyakazi na Vyama vya Waajiri wa Mwaka 2025,Mwongozo wa Uratibu wa Vyama vya Watu Wenye Ulemavu wa Mwaka 2025, na Mwongozo wa Wakala Binafsi wa Ajira wa Mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment