
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Mbaruku Magawa, amesema waajiri ni wadau namba moja katika utekelezaji wa majukumu ya Mfuko.
Ameyasema hayo Agosti 7, 2025, wakati wa kikao kazi baina ya Mfuko na wawakilishi wa waajiri wa mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.
“ Mfuko unajibadilisha, unajaribu kurahisisha upatikanaji wa huduma zeke, ili kurahisisha huduma, mdau namba moja ambaye ni mwajiri ni mtu muhimu sana, kwasababu wakati mwajiriwa anapoanza ajira, huwa tunafanya kazi kwa karibu nanyi,” alisema
Alisema ushirikiano baina ya Mfuko na waajiri unaanza wakati wa zoezi la kusajili wafanyakazi wanapoanza ajira, kwenye masuala ya kuhuisha kumbukumbu za wanachama, kuwasilisha michango (asilimia 100 linawaangukia waajiri), masuala ya kuwasilisha madai, na hata masuala ya kubooresha mafao ya wanachama.” Alisisitiza Bw. Magawa.
Kuhusu huduma za Kidijitali, Mkurugenzi huyo wa Uendeshaji PSSSF, alisema lengo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma, kutoa huduma ambayo ni sahihi lakini pia kupunguza udanganyifu.
Waajiri wanayo njia ya ufikiaji (Access) mifumo ya PSSSF na Sheria yetu inawapa ninyi waajiri jukumu la kuleta kumbukumbu za wanachama, kuleta michango, jukumu la kuhakikisha vitu vyote vinavyowasilishwa kwenye mfuko viko sahihi, hivyo tumewaletea mfumo ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yote hayo. Alisisitiza Bw. Magawa.




No comments:
Post a Comment