WATU ZAIDI YA 5,000 WAPATIWA MSAADA WA KISHERIA NANENANE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 11, 2025

WATU ZAIDI YA 5,000 WAPATIWA MSAADA WA KISHERIA NANENANE


‎Na Edward Winchislaus.

‎Watu zaidi Elfu tano wamepatiwa msaada wa kisheria katika banda la wizara ya Katiba na sheria katika maonesho ya nanenane yaliyofanyika Nzuguni Jijini Dodoma tangu Agosti 1 hadi Agosti 10.2025.

‎Hayo yameelezwa Agosti 10.2025 na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya katiba katika wizara hiyo Bw.Prosper Kisinini wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya nanenane jijini Dodoma.

‎Amesema Kati yao wanawake walikuwa zaidi ya 3,000 huku wanaume walikuwa zaidi ya 2,000 na migogoro zaidi ya 100 imetatuliwa.

‎"Wizara ya katiba na sheria imetoa msaada wa kisheria kwa watu zaidi 5,526 ambapo wanawake walikuwa zaidi ya 3,408 na wanaume zaidi ya 2,473 na kushughulikia migogoro 103,"amesema.

‎Katika hatua nyingine Katibu mkuu wa wizara ya katiba na sheria Bw.Eliakim Chacha Maswi mewapongeza watendaji wa wizara hiyo kwa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi hao.








No comments:

Post a Comment