
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Ubalozi wa Iran nchini Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran, Dkt. Mohsen Maarefi na kujadiliana mashirikiano katika Sekta ya Malikale, Utalii na mafunzo.
Kikao hicho kilichofanyika leo Agosti 5,2025 jijini Dar es Salaam kimejadili namna ya kushirikiana katika eneo la utafiti wa malikale, teknolojia ya uhifadhi katika makumbusho za taifa za nchi hizo mbili pamoja na kuwa na onesho la pamoja la historia ya watu wa Iran nchini Tanzania.
Kuhusu sekta ya utalii kikao hicho kimejadili namna bora ya kuvutia watalii wengi kutoka nchi Iran hasa kupitia Halal Tourism ambapo Tanzania itapata mafunzo ya namna bora ya kuandaa vyakula vya ki-Iran ili kuvutia watalii hao.
Aidha, Tanzania kujiweka katika nafasi ya kulikamata soko la Iran kwa kutangaza maeneo yenye historia ya pamoja kama Kilwa, Kunduchi, Zanzibara baadhi ya maeneo mengine.
Sambamba na hayo, kikao hicho kimeona umuhimu wa nchi hizo mbili kushirikiana katika eneo la mafunzo kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii kwa kuanzisha program ya kubadilishana uzoefu baina ya maprofesa wa Tanzania na Iran.





No comments:
Post a Comment