BASHUNGWA AKUTANA NA ASKOFU BAGONZA; WACHUNGAJI WAOMBEA AMANI NA MAFANIKIO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 5, 2025

BASHUNGWA AKUTANA NA ASKOFU BAGONZA; WACHUNGAJI WAOMBEA AMANI NA MAFANIKIO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI.



Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, pamoja na Wachungaji na viongozi wa kanisa hilo, leo tarehe 5 Septemba 2025, wamekutana na kuzungumza na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karagwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Innocent Bashungwa. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za KKKT zilizopo Rukajenge, Karagwe, muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa CCM Wilaya ya Karagwe.

Baada ya mazungumzo hayo, Askofu Dkt. Bagonza ameongoza maombi ya kuliombea Taifa, uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025, na kampeni za vyama vya siasa. Vilevile, amemtakia heri Ndugu Bashungwa katika harakati zake za kisiasa na kuwataka wananchi kuendeleza mshikamano na mshikamani katika kipindi hiki cha uchaguzi.




No comments:

Post a Comment