
"Kasi ileile tuliyoenda nayo miaka mitano iliyopita ni kasi ileile tutakayoenda nayo kwenye miaka mitano ijayo kwenye sekta ya elimu, afya, miundombinu, maji lakini pia umeme, tunataka kila Mtanzania aguswe na vitu hivyo awe na maji safi na salama, watoto wapate fursa ya kusoma msingi mpaka sekondari mpaka vyuo lakini juu ya hilo tumejenga vyuo vya Ufundi, Vijana wetu hawa, wenyewe wanajiita masela wapate maeneo ya kwenda kuongeza ujuzi kwa kazi wanazozifanya."
Lakini pia tunataka kila Mtanzania afikiwe na huduma ya afya na kwa yule asiyekuwa na uwezo tumesema serikali itakwenda kumsaidia lakini kila Mtanzania apate huduma za afya. Tunataka Kila Mtanzania aone umeme utakaomsaidia kurahisisha kazi zake nyumbani, kufanya shughuli zake za kiuchumi, lakini pia kulinda usalama wa maeneo yetu. Umeme ni usalama wa maeneo yetu."
"Ujenzi wa miundombinu ni shughuli nyingine muhimu kwa uchumi wetu na hapa nimesikia kilio cha barabara, nataka niseme kwamba tunajipanga, jinsi tutakavyoweza na Mungu atakavyotuwezesha kuzijenga barabara za Tanzania yote. Hatutamaliza kwa miaka mitano ijayo lakini kazi kubwa tutaifanya katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, lengo letu ni kurahisisha usafirishaji na usafiri wa watu na bidhaa, bidhaa zisafirishwe zifike masokoni lakini na watu waweze kusafiri kwa haraka ili kwenda kufanya shughuli zao za kiuchumi, shughuli za kijamii lakini pia za kisiasa." Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza na wananchi wa Mafinga Mkoani Iringa leo Jumamosi Septemba 06, 2025.




No comments:
Post a Comment