DKT. SAMIA AAHIDI KUENDELEZA MIUNDOMBINU NA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WANANCHI WA UVINZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 13, 2025

DKT. SAMIA AAHIDI KUENDELEZA MIUNDOMBINU NA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WANANCHI WA UVINZA


Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Chs Mapinduzi CCM ameahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii Wilayani Uvinza, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya elimu pamoja na afya.

Dkt. Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Septemba 13, 2025 wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, akisisitiza pia haja ya kuendelea na sera ya elimu bila ada ikiwa atachaguliwa kuendelea kuiongoza Tanzania katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025

Ameahidi kujenga vituo vya afya vya Kadanga, Kabeba, Kazuramimba na Basanza, kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Msihezi, Lagosa, Sambala, Rulinga na Kahubili, akitangaza pia kuanza kwa zoezi la majaribio ya utekelezaji wa bima ya afya kwa wote ndani ya siku mia moja za mwanzo ikiwa atachaguliwa kuongoza serikali.

Akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika awamu yake ya kwanza ya Uongozi kwenye Wilaya hiyo, Dkt. Samia amesema serikali yake imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa dawa kwa asilimia 11 na hivyo upatikanaji wa dawa Wilayani humo kufikia asilimia 91 pamoja na utoaji wa Bilioni 13 zikitumika pia kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwenye shule za msingi ikiwemo ujenzi wa shule 34 mpya.

Aidha Shilingi Bilioni 19 pia zilitolewa kujenga shule mpya za Sekondari, suala ambalo limewezesha Wilaya ya Uvinza kuwa na shule za sekondari 31, akisema ujasiri walionao sasa mbele ya wapigakura ni kutokana na mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka minne ya serikali yake ya awamu ya sita.


No comments:

Post a Comment