
Dkt. Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM amesema Ikiwa atachaguliwa kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, serikali yake itaendelea kuvutia zaidi wawekezaji kuwekeza Mkoani Kigoma ili kuufanya Mkoa huo kuwa Kitovu cha biashara kwa Ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Septemba 13, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Kasulu Mjini wakati wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM, akisema uwepo wa umeme wa uhakika, Reli ya kisasa ya SGR pamoja na reli ya Kati Mkoani humo ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya kiuwekezaji, akiwasihi wananchi kujiandaa na kutumia vyema fursa za ujio wa Miundombinu hiyo pamoja na Viwanda vinavyojengwa Mkoani humo.
Kulingana na Dkt. Samia, Kigoma ndio Mkoa pekee utakaokuwa na vituo vingi vya reli ya SGR akisema upekee huo utasababisha Mkoa huo kuwa kitovu cha biashara kati yake na nchi jirani, ukiwa pia ni Mkoa wa Kimkakati katika uzalishaji wa sukari na saruji nchini.




No comments:
Post a Comment