DKT. SAMIA KUBISHA HODI PEMBA LEO, KUZISAKA KURA ZA USHINDI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 20, 2025

DKT. SAMIA KUBISHA HODI PEMBA LEO, KUZISAKA KURA ZA USHINDI


Baada ya kuhitimisha kampeni zake za siku Mbili Unguja visiwani Zanzibar, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi Septemba 20, 2025 anaendelea na Kampeni zake Pemba, akitarajiwa kuomba kura na kuinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu kwenye Mkutano wa hadhara Gombani ya Kale.

Awali Dkt. Samia amekuwa na mikutano yake ya kampeni Makunduchi, Kusini Unguja na baadaye Nungwi, Kaskazini Unguja, akiahidi kukuza uchumi na Kipato cha mwananchi mmoja mmoja huku pia akisisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuwajibika katika kuhakikisha kila mwananchi anapata mahitaji muhimu kwa katika kulinda utu wa Mtanzania pamoja na kuendelea kuimarisha upatikanaji wa ajira kwa Vijana kwa kuzalisha angalau ajira 350, 000 kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Katika Ilani ya CCM ya 2025/30 Dkt. Samia kwa Pemba pamoja na mambo mengine ameelekezwa kuendeleza kiwanja cha ndege cha Pemba kwa Kuongeza urefu wa njia ya kurukia ndege (Run way) na ujenzi wa jengo jipya la abiria, kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwemo Karafuu, Makonyo na Mwani pamoja na kuboresha ustawi wa jamii na kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa yanayozuilika, kuinua wananchi kiuchumi na kuleta utulivu na ustawi wa jamii ya Wazanzibar pamoja na kuanzisha hifadhi ya Taifa ya chakula, hifadhi ya Taifa ya mafuta ya Petroli na dizeli kwa lengo la kuhakikisha uendelevu wa upatikanaji wake na kupunguza athari za mabadiliko ya bei ya bidhaa hizo.

Kulingana na Dkt. Samia, mazingatio mengine maalumu ya Zanzibar na maeneo makuu ya utekelezaji itakuwa ni sambamba na kuchochea mapinduzi ya uchumi wa kisasa na endelevu, kuongeza fursa za ajira, kuchochea mapinduzi ya kidigitali pamoja na kuweka vivutio maalumu vya kushajihisha uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta kuu za kiuchumi ambazo ni uchumi wa buluu, kilimo, viwanda na huduma visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment