
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, akiwasili kwenye Kijiji cha Kalenga, Jimbo la Kalenga Mkoani Iringa kwaajili ya Mkutano wake wa Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Kulingana na Chifu wa Kabila la Wahehe Chifu Abdul Sapi Mkwawa Dkt. Samia ambaye pia ni Rais wa awamu ya sita wa Tanzania ni Kiongozi wa Pili kufika kwenye Kijiji hicho, wa kwanza akiwa ni Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Kijijini hapo kushiriki mazishi ya Chifu Mkwawa.


No comments:
Post a Comment