MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwahutubia Wananchi kwenye Mkutano wake wa Kampeni leo Ijumaa Septemba 12,2025 katika Uwanja wa Soweto, jijini Arusha.
Akiwa katika mkutano huo Dkt Nchimbi pia alipata wasaa wa kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo, akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Ndugu Paul Christian Makonda pamoja na madiwani.
Aidha Dkt. Nchimbi pia aliongoza uzinduzi wa mikutano ya kampeni kwa Jimbo la Arusha Mjini mbele ya Wananchi waliofika kumsikiliza.
Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.
Dkt. Nchimbi siku ya leo ameanza kufanya mikutano ya kampeni mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa kuanzia Arusha ambapo amefanya mikutano mitatu akianzia Longido, Arumeru Magharibi na kumalizia Arusha Mjini huku umati wa wananchi ukitoa ahadi ifikapo siku ya uchaguzi wao wanatiki kwa wagombea wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment