Ikulu na Menejimenti ya Utumishi wa Umma mabingwa SHIMIWI 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 16, 2025

Ikulu na Menejimenti ya Utumishi wa Umma mabingwa SHIMIWI 2025


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Timu za Ofisi ya Rais Ikulu na Menejimenti ya Utumishi wa Umma wametetea ubingwa wao katika mchezo wa mpira wa netiboli na soka katika michuano ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) iliyofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Ikulu timu tishio inayoundwa na wachezaji mahiri wameweza kutetea ubingwa wao kwa kushinda mechi za kuanzia hatua za makundi, baadaye 16 bora, robo fainali, nusu fainali na hatimaye fainali wamewafunga Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kwa magoli 72-18.

Ikulu yenye wachezaji wenye kucheza kwa kuonana waliweza kumaliza robo ya kwanza wakiwa mbele kwa magoli 19-4, na baadaye kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli 36-12 na robo ya tatu kwa magoli 63-13.

Kwa upande wa soka timu ya Utumishi imetwaa ubingwa baada kuwafunga Tume ya Umwagiliaji kwa magoli 4-2 katika mchezo mkali wa fainali uliomalizika kwa sare ya 1-1 katika hatua za awali na baadaye wakapigiana penalti, ambapo mabingwa watetezi walifanikiwa kushinda 3-1 na kufanya jumla ya magoli yaliyowapa ushindi kuwa 4-2.

Awali Mwenyekiti wa klabu ya Utumishi, Bw. Charles Shija alijihakikishia kutetea ubingwa wake, kutokana na kuwa na kikosi mahiri na kilichofanikiwa kufanya vyema kuanzia hatua ya makundi hadi fainali.

Ushindi wa tatu kwa upande wa mpira wa miguu ulikwenda kwa Taasisi a Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU waliowafunga Wizara ya Katiba na Sheria kwa bao 1-0; na kwa upande wa netiboli Utumishi waliwafunga Wizara ya Maliasili na Utalii kwa magoli 71-19.

Awali kabla ya mchezo wa fainali kulitanguliwa na mchezo kati ya Viongozi wa SHIMIWI dhidi ya Veteran wa Mwanza, ambapo viongozi walifungwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment