
📌 REA yapongezwa utekelezaji kampeni ya nishati safi ya kupikia
Na Mwandishi Wetu, Chato, GEITA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewahamasisha wananchi kuunga mkono kampeni ya nishati safi ya kupikia ili kulinda afya pamoja kuokoa mazingira.
Ussi ametoa wito huo jana Septemba 6, 2025 wakati wa ugawaji wa mitungi ya gesi ya kilogramu 6 zaidi ya 500 kwa wananchi wa Wilaya ya Chato, Mkoani Geita inayotolewa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umelenga kufikia mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati ya kupikia.

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya hiyo wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia REA kwa kuwapatia majiko ya gesi huku viongozi wa Kijiji wakiahidi kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wao.
“Mimi kama Kiongozi nitaendelea kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake watumie nishati safi ya kupikia kama gesi.
Lakini pia nitaunda kamati ya kupita katika kila Kitongoji kuhamasisha wananchi ambao wanatumia kuni waanze kutumia nishati safi ya kupikia,” amesema Juma Nzihilabike, Mwenyekiti wa Kijiji cha Musasa.
Kwa upande wake Mhandisi Miradi kutoka REA, Francis Manyama amesema kuwa REA inaendelea kutekeleza maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwamo mradi wa kugawa majiko ya gesi pamoja na majiko banifu kwa bei ya ruzuku.












No comments:
Post a Comment