
MAANDALIZI ya mikutano ya kampeni ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, mkoani Ruvuma yamekamilika.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amethibitisha hilo leo Septemba 20, baada ya kukagua maandalizi hayo akiwa ameambatana na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika kwa ajili ya kumpokea mgombea huyo.
Kwa mujibu wa Oddo, Dkt. Samia anatarajiwa kuwasili kesho Septemba 21 katika Uwanja wa Ndege wa Songea, ambapo atapokelewa na Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel John Nchimbi, viongozi wa chama pamoja na wananchi wa mkoa huo.
Ziara yake itaanzia wilayani Nyasa, ikiwemo kusimama Mbinga kuzungumza na wananchi na kisha kufanyika mkutano mkubwa wa kampeni katika eneo la Mbamba Bay.
Aidha, Septemba 22 Dkt. Samia atahutubia mkutano mkubwa wa kampeni mjini Songea katika Viwanja vya VETA vilivyopo Msamala, kabla ya kuelekea Namtumbo na Tunduru ambapo atafunga ziara yake ya kampeni mkoani humo.
Baada ya hapo, Septemba 23 ataanza kampeni mkoani Mtwara.








No comments:
Post a Comment