
Maelfu ya wananchi wa Chake Chake Unguja Visiwani Zanzibar wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM leo Septemba 20, 2025 kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale, ikiwa ni siku yake ya kwanza ya Kampeni Pemba. Dkt. Samia ametumia Mkutano wake kuwatoa hofu wananchi wa Pemba, akiwahakikishia wananchi usalama wa kutosha siku ya kupiga kura Oktoba 29, 2025 na kusema Vikosi vya ulinzi na usalama vimejipanga vyema kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kushiriki na kupiga kura kikamilifu.









No comments:
Post a Comment