
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 20, 2025 akiwa Pemba, Zanzibar kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale wilayani Chake Chake, ameahidi kujenga uwanja wa ndege wa Pemba ikiwa atachaguliwa katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, katika jitihada za kuifungua Pemba kibiashara na kiuchumi kwa kuvutia uwekezaji na shughuli za kiuchumi na Kijamii.
Dkt. Samia akihutubia Mamia ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya Kampeni Visiwani Pemba leo Septemba 20, 2025, Dkt. Samia pia amesema katika mpango wa serikali, Uwanja huo utakuwa wa kimataifa na utawezesha wafanyabiashara pia kutumia uwanja huo katika usafirishaji wa mizigo kutoka nje ya nchi kwenda kisiwani humo.
Aidha Dkt. Samia ameahidi kuwa serikali yake itamalizia ujenzi wa barabara ya Chake- Mkoani, akisema fedha ipo sambamba na ya Ujenzi wa bandari ya Wete ambayo itajengwa kwa kutumia fedha za Mkopo kutoka Korea Kusini, zikiwa ni jitihada za serikali ya awamu ya sita, iliyopambana kupata fedha hizo kutoka kwa wahisani hao.



No comments:
Post a Comment