
Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza ratiba ya kukabidhi rasmi Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 – 2030 pamoja na uzinduzi wa kampeni za Ubunge katika Jimbo la Segerea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama hicho, Shangwe Ayo, tukio la kukabidhiwa kwa ilani litafanyika Septemba 22, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hakainde Hichilema, Makao Makuu ya Chama, Magomeni, kuanzia saa 5:00 asubuhi.
Mgeni rasmi atakuwa Kiongozi wa Chama, Ndugu Dorothy Semu, akifuatana na viongozi wakuu wengine.
Baada ya tukio hilo, viongozi hao watashiriki mkutano wa kampeni katika Jimbo la Segerea, ambako wagombea wa ubunge na udiwani wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Mkoa wa Mwambao (kikanda) watatambulishwa. Mkutano huo utarushwa mubashara na vyombo mbalimbali vya habari kuanzia saa 9:00 mchana hadi saa 12:00 jioni.
ACT Wazalendo imesisitiza kuwa katika matukio hayo, chama kitatoa “uamuzi mzito” kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa nchi. Kaulimbiu ya chama inabaki kuwa: “Tunapambana Tukishiriki, Tunashiriki Tukipambana. Taifa Kwanza Leo na Kesho.”
No comments:
Post a Comment