Na Oscar Assenga,TANGA
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia (CUF) Samandito Gombo amesema siku 100 baada ya kuchaguliwa kuwa Rais atahakikisha anaanzisha mchakato wa katiba mpya na itakuwa ni siku ya kwanza baada ya kuapishwa.
Gombo aliyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Tanga ambapo alisema atateua tume ya kuanza kushughulika na suala la katiba mpya kwa sababu ndio mama wa kila jambo na demokrasia ya nchi kama wanataka iende vizuri.
Alisema kwamba kama wanataka iende vizuri ni lazima kuwe na sheria ambayo imeiweka vizuri nchi na sio suala la kukaa kila wakati wanabishana kwa kuongelea jambo bila kutekeleza na ndani ya siku hizo kuna sheria nyingi zitabadilika.
“ Kwa mfano sheria za utumishi wa umma zitabadilika ziweze kufanya mambo yanayoweza kudhibiti mali za umma na kuwafanya wafanyakazi wa umma waweze kufanya kazi zao vizuri lakini pia nitafuta kikokotoo na wafanyakazi hawatalipa mambo mengine ndio watasubiri muda mrefu.
Akizungumzia suala la ajira alisema kwamba watakapoingia ajira wataziba magepu yaliyopo na watachukua watu wote wenye sifa kwa kuangalia mageupu huku akieleza kwamba huduma za Serikali zitatolewa kwenye ngazi ya kata na hazitatolewa kwenye Halmashauri watakaoajiriwa watakwenda kufanya kazi ndani ya kata ili wananchi waweze kupata huduma kwenye ngazi ya kata.
Mgombea Urais huyo wa CUF yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya Kampeni ambapo anatembelea wilaya mbalimbali mkoani Tanga
No comments:
Post a Comment