MITAMBO YA KUCHIMBA VISIMA YAANZA KAZI BONDE LA MZAKWE - DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 4, 2025

MITAMBO YA KUCHIMBA VISIMA YAANZA KAZI BONDE LA MZAKWE - DODOMA



Wizara ya Maji imeelekeza Mitambo ya kuchimba maji ielekezwe katika Bonde la Maji Mzakwe kuchimba visima viwili vyenye urefu wa mita 150 kila kimoja, ikiwa ni jitihada za serikali kuongeza vyanzo vipya vya maji ili kukidhi mahitaji katika Jiji la Dodoma.

Serikali imetoa kiasi cha shilingi Milioni 300 kugharamia uchimbaji wa visima hivyo kuhakikisha Mpango wa serikali wa muda mfupi wa kuchimba visima vya maji pembezoni mwa Jiji la Dodoma unatekelezwa ili huduma ya maji ipatikane kwa uhakika kwenye maeneo yenye changamoto ya maji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amesema kazi ya uchimbaji wa visima katika Bonde la Mzakwe itasaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutokana na baadhi ya visima kushuka uwezo wa kuzalisha maji.

Aidha Mhandisi Aron amewaomba wananchi wa maeneo yaliyoathirika na changamoto ya kushuka kwa uzalishaji katika chanzo cha maji cha Mzakwe kwamba huduma itaimarika baada ya kazi hiyo kukamilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Simon Mamba ameitaka DUWASA kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaj Jabir Shekimweri amepongeza Jitihada zinazochukuliwa na Wizara ya Maji kwa kushirikisha Taasisi zake kutafuta suluhu ya changamoto ya maji katika Jiji la Dodoma.

Uchimbaji wa visima viwili vya maji katika Bonde la Mzakwe utakamilika ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment