DKT JINGU AZINDUA KAMATI YA MAKAO YA TAIFA YA WATOTO KIKOMBO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 4, 2025

DKT JINGU AZINDUA KAMATI YA MAKAO YA TAIFA YA WATOTO KIKOMBO.



Na WMJJWM-Dodoma.


Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki kwa ajili ya ustawi wa watoto nchini kupitia utekelezaji na uimarishaji wa afua mbalimbali hususan watoto waliotokea katika mazingira magumu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu katika uzinduzi wa Kamati ya makao ya Taifa ya Watoto Kikombo Septemba 04, 2025 Katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.

Dkt. Jingu ameeleza kwamba uwepo wa Kamati hiyo ni moja ya uimarishaji wa afua ya kuboresha ustawi wa watoto hasa waliotokea katika mazingira magumu ili kuhakikisha wanapata malezi na makuzi stahiki kama yale yanayopatikana watoto waliopo kwenye familia ili waweze kufikia utimilifu wao kupata taifa bora.

“Sote tunafahamu kuwa sehemu sahihi na muhimu ya kumlelea mtoto ni kwenye familia lakini sababu ya changamoto mbalimbali baadhi ya watoto hujikuta kulelewa kwenye familia imeshindikana na hapo ndipo nguvu ya taifa inaingia ili kuhakikisha watoto hao wanapatiwa malezi yanayotakiwa ikiwemo kuwaanda kukabiliana na changamoto mbalimbali za dunia ili wanapofikia umri wa kujitegemea waweze kumudu kuendesha maisha yao” amesema Dkt. Jingu.

Aidha Dkt Jingu ametoa rai kwa Kamati hiyo kuhakikisha inaongeza thamani katika makao hayo kwa kuja na mikakati mizuri zaidi ya kuwalea watoto hao na kuwafikisha katika utimilifu wao.

“Inabidi mje na ushauri na mawazo yatakayo weza tusaidia kwenda mbele na kuboresha makao hayo hata yaweze kuwa ya mfano kwa makao mengine ya kulelea watoto nchini kwani Wizara ipo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha utakao wawezesha kufanya kazi yenu vizuri.”amesema Dkt Jingu.

Naye Mwanakamati Josephine Mwaipopo ambaye ni Afisa Ustawi wa Mkoa wa Dodoma amesema kwamba makao hayo yamekua mfano mzuri na wa kuigwa kwa makao ya kulelea watoto nchini kwani yana vigezo sahihi vya marejeo hata kwa wamiliki wa vituo na makao binafsi hivyo ni jukumu la Kamati kuhakiksha makao hayo yanazidi kuwa bora.

Kwa Upande wake mwanakamati kutoka Abbot Fund Alfred Magala amesema wadau hao wako tayari kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuweza kusukuma ustawi wa watoto na jamii kwa ujumla .

Kamati hiyo yenye wajumbe 12 ikiongozwa na Deodatus Orotha ambae ni Mkuu wa chuo cha Veta inatarajia kufanya kazi kwa muda wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment