
WADAU wa maendeleo Mkoa wa Morogoro,wamempongeza mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi,Rais Samia Suluhu kwa ahadi 13,atakazotekeleza ndani ya siku 100 baada ya kuchaguliwa kuongoza nchi kwa awamu ya nyingine.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Tanzania Initiative for Social and Economic Relief (TISER),na Mwenyekiti wa NaCoNGO mkoa wa Morogoro Otanamusu Nicholas wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro.
Nicholas anasema Mgombera Urais kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu ameleta matumaini makubwa kwa wakazi wa morogoro na Tanznia kwa ujumla kwani utekelezaji wa ahadi utafanyika na kuleta matokeo mazuri ndani ya nchi.
“Ahaidi 13 alizotoa Mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu zitatimia kwani yeye yupo madarakani,,na ahadi nyingine zinafanyiwa kazi chini ya uongozi wake,sina shaka na hilo kabisa”Anasema Nicholas.
Aidha anasema wananchi wanapaswa kumtia moyo mgombea huyo,kwani ana nguvu ya utekelezaji na kuendelea kushirikiana na serikali yake iliyopo madarakani na itakayokuja kwa lengo la kutimiza ahadi hizo kwa asilimia mia moja.
Pia anasema Mgombea huyo kupitia chama cha Mapinduzi aliahidi kujenga soko la kisasa mkoani Morogoro,jambo hili litaleta faraja kubwa kwa wafanyabiashara kwani litasaidia kukuza uchumi wa mkoa na mwananchi mmoja mmoja.
Katika ahadi hizo upande wa afya,serikali itapiga marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia miili ya Marehemu kuchukuliwa na ndugu zao hata kama gharama za matibabu aliyopatiwa marehemu hazijalipwa,serikali itakuja na mfumo mwingine wa kuhakikisha jamaa wa marehemu wanalipa gharama hizo.
Serikali itaanza kugharimia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo Saratani, Figo, Moyo, Sukari, Mifupa na Mishipa ya Fahamu.

No comments:
Post a Comment