
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kupitia kikosi cha usalama Barabarani limewaongezea maarifa ya matumizi sahihi ya barabara madereva wa serikali Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa lengo kusaidia kupunguza ajali za barabarani kwa watumiaji wote.
Akizungumza na madereva hao Septemba 25, 2025 katika Mji wa Serikali Mtumba Wizarani hapo Sajent wa Polisi Ester Makali kutoka dawati la elimu ya usalama barabarani amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuheshimu alama za barabarani na kuchukua tahadhari.
Vilevile, Makali amewaasa madereva hao kutokuwa sehemu ya madereva wanaovunja sheria kwa kuendesha mwendo kasi bila kuchukua tahadhari na kutokuheshimu watumiaji wengine wa barabara jambo ambalo limekuwa likinyoshewa vidole na wananchi.
Aidha, amewataka madereva kuonyesha mabadiliko kupitia elimu iliyotolewa na Jeshi la Polisi kwa kuwa mabalozi wa kuzuia ajali za barabarani huku wanufaika wa elimu hiyo wakiahidi kuendelea kutii sheria za usalama barabara na kutoe elimu hiyo kwa madereva wengine.









No comments:
Post a Comment