Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kulia) wakikata utepe wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameongoza uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara hatua inayolenga kusaidia uwezeshaji wa wafanyabiashara katika ngazi zote.
Akizungumza Jumatano Septemba 10, 2025 wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mhita amesema dawati hilo limeanzishwa na TRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa lengo la kuwatambua, kuwasikiliza na kuwawezesha wafanyabiashara ili kukuza mitaji na kuongeza tija katika biashara zao.
Mhita amebainisha kuwa dawati hilo litakuwa daraja la kuwaunganisha wafanyabiashara na taasisi za kifedha ili kupata mikopo kwa urahisi zaidi pamoja na kuwaongoza katika njia bora za urasimishaji biashara.
Aidha, ameeleza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuwatambua na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo ili wachangie kikamilifu katika kukuza uchumi wa Taifa.
“Lengo letu ni kuhakikisha kila mfanyabiashara, mdogo kwa mkubwa, anatambulika rasmi na anapata msaada unaohitajika. Dawati hili litakuwa ni nyenzo muhimu ya kuwafikishia huduma karibu, kutoa elimu ya biashara na kusikiliza changamoto zao,” amesema Mhita.
Aidha Mhe. Mhita, amesema kuwa, kuanzishwa kwa dawati hili ni fursa ya kipekee ya kuimarisha mazingira ya biashara mkoani Shinyanga, hatua itakayosaidia kuongeza mapato ya Serikali, kukuza ajira na kuimarisha uchumi wa wananchi.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro, amesema TRA itahakikisha inaishi katika dhima ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutoa huduma bora kwa wafanyabiashara wote, bila kuangalia ukubwa wa biashara zao na kwamba mamlaka hiyo itaendelea kusikiliza na kuzifahamu changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika sekta mbalimbali.
"Dawati hili maalum lina jukumu la kusaidia kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara katika sekta isiyo rasmi ili waweze kusajiliwa, kutambuliwa na hatimaye kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali. Kwa mujibu wa takwimu, sekta isiyo rasmi inachangia zaidi ya asilimia 30 ya pato la Taifa na kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania milioni saba. Hivyo basi, ni muhimu kuhakikisha kundi hili linawezeshwa ipasavyo. Kwa niaba ya TRA Mkoa wa Shinyanga, nawahakikishia ushirikiano wa dhati na huduma bora kwa kila mfanyabiashara",amesema Maro.
"Tumeanzisha dawati hili kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ambaye ametoa maelekezo kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha huduma bora na jumuishi kwa wafanyabiashara wote. Katika Mkoa wa Shinyanga, dawati hili limeanzishwa katika ofisi ya TRA ya mkoa pamoja na katika kila wilaya ili kuhakikisha huduma inapatikana kwa urahisi na kwa ukaribu zaidi",ameongeza.
Ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza na kutumia huduma za dawati hili ili kujisajili, kupata elimu ya kodi, na kushirikiana na TRA kwa karibu na kwamba TRA iko tayari kuwafuata mahali walipo ili kutambua mahitaji na changamoto zao, na kuhakikisha wanapata msaada wa haraka.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa Serikali, Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, wawakilishi wa TCCIA, wafanyabiashara, pamoja na wadau wa sekta binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara leo Jumatano Septemba 10, 2025 katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara leo Jumatano Septemba 10, 2025 katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara leo Jumatano Septemba 10, 2025 katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro akizungumza wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro akizungumza wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita na Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Maro (kulia) wakifurahia baada ya kukata utepe wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita (aliyekaa kushoto) akiwa kwenye chumba cha Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita (katikati) akikata keki wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita (katikati) akikata keki wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.


Keki maalumu wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.
Keki maalumu wakati uzinduzi wa Dawati Maalum la Uwezeshaji Biashara Mkoa wa Shinyanga.


No comments:
Post a Comment