RPC, HYERA AZINDUA UJENZI WA KITUO CHA POLISI ITOLOLO KIMBURY - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 10, 2025

RPC, HYERA AZINDUA UJENZI WA KITUO CHA POLISI ITOLOLO KIMBURY



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (Acp), Galus Hyera Septemba 10, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Polisi kimbury Itololo kilichopo katika kata hiyo wilaya kondoa jijini Dodoma.

Kituo hicho ambacho kimejengwa na familia ya Padre Paul Mhindi kimekabidhiwa kwa Jeshi la Polisi sambamba na sherehe ya jubelei ya miaka 25 ya upadre ya Padre Paul Mhindi.

Padre Mhindi amesema familia hiyo imekua na desturi ya kufanya matendo ya huruma kwa jamii na kufikia uamuzi wa kutambua umuhimu wa Jeshi la Polisi katika kuzuia na kutanzua uhalifu, na kuunga mkono jitihada hizo kwa kukabidhi jengo pamoja na eneo ili kuhakikisha jamii inakuwa salama kiroho na maisha ya watanzania yanakua salama bila uhalifu.

Kwa niaba ya mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP) camillius Wambura Kamanda Hyera, ameipongeza familia hiyo kwa hatua zilizofikiwa za ujenzi wa kituo hicho na kuahidi kuunga mkono jitihada za ukamilishwaji kituo hicho pamoja na kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika kata ya Itololo na maeneo jirani.

Aidha Hyera amesema uwepo wa kituo hicho kutasaidia wananchi wa kata hiyo kuto kutembea umbali mrefu kutatua changamoto za kiusalama, na kuwasisitiza wananchi kufuata sheria na kuripoti matukio ya uhalifu ili yaweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wao wanufaika wa kituo hicho wamepongeza Jeshi la Polisi kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo ya kiusalama yanayofanywa na wananchi na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kuwabaini wahalifu kwa kutoa taarifa mapema kabla uhalifu haujatendeka.







No comments:

Post a Comment