
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mchinga, mkoani Lindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Salma Rashid Kikwete, amezindua rasmi kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Uzinduzi huo umefanyika leo katika Kata ya Rutamba, Manispaa ya Lindi, na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.








No comments:
Post a Comment