Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Michezo ya vishale (DARTS) na bao imetoa mabingwa wapya kwenye michezo ya 39 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI), iliyofanyika kwenye Bwalo la Magereza Butimba jijini Mwanza.
Katika mchezo wa vishale kwa wanawake bingwa mpya ni mchezaji Eliasenya Nnko kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kamshinda Adeline Nyoni wa TSC katika mchezo wa fainali; huku Imani Wabu kutoka Wizara ya Uchukuzi aliibuka wa tatu baada ya kumshinda Eunice Chengo wa Mahakama.
Kwa upande wa wanaume bingwa mpya ni Fortunatus Benedict wa Wizara ya Maji ametwaa ubingwa kwa kumfunga Benedict Mombeki wa Wizara ya Ardhi; wakati ushindi wa tatu umechukuliwa na Hassan Ligoneko wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma aliyemshinda Anthony Luoga wa RAS Ruvuma.
Katika mchezo wa bao kwa wanawake bingwa mpya ameibuka Jamila Kalambo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi aliyemshinda Laina Abbas wa Wizara ya Maji; naye Filomena Haule wa Mahakama ameshika nafasi ya tatu kwa kumfunga Mwabibi Bakari wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Kwa upande wa wanaume bingwa mtetezi pekee ametetea ubingwa wake ni Emmanuel Komba wa RAS Ruvuma aliyemshinda mwenyeji Wambura Mgaya wa RAS Mwanza; wakati ushindi wa tatu umechukuliwa na Adam Nyando wa Wizara ya Mambo ya Ndani aliyemfunga Omar Mataka wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Michezo hii ya SHIMIWI itaendelea kesho tarehe 13 Septemba, 2025 kwa michezo ya Karata, na nusu fainali ya kuvuta kamba, mpira wa miguu na netiboli, ambayo itafanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 12 asubuhi.

No comments:
Post a Comment