TAKUKURU SPORTS CLUB YAKABIDHI MAKOMBE YA USHINDI KWA MKURUGENZI MKUU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 19, 2025

TAKUKURU SPORTS CLUB YAKABIDHI MAKOMBE YA USHINDI KWA MKURUGENZI MKUU


Klabu ya Michezo ya TAKUKURU imemaliza mashindano ya michezo ya 39 ya SHIMIWI kwa kuibuka 'Mshindi wa Jumla' katika Michezo ya 39 ya SHIMIWI na kukabidhi kwa Mkurugenzi Mkuu, vikombe na medali zilizopatikana.

Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu katika hafla iliyofanyika Septemba 18, 2025 TAKUKURU Makao Makuu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Neema Mpembe Mwakalyelye, amewapongeza wanamichezo kwa kufanya vizuri katika mashindano na kupata ushindi mkubwa uliosababisha TAKUKURU kupata ushindi wa Jumla wa Mashindano ya SHIMIWI mwaka 2025.

Bibi Neema alisema kuwa matokeo mazuri na ushindi uliopatikana umeitangaza vema TAKUKURU kwa sababu mara zote timu zilipopata ushindi TAKUKURU ilitangazwa katika vyombo mbalimbali vya Habari.


Kutokana na ushindi huo TAKUKURU imepata jumla ya vikombe sita kama ifuatavyo: -

📌Mshindi wa Jumla wa Mashindano, 
📌Mshindi wa Jumla wa Riadha, 
📌Mshindi wa Kwanza wa Baiskeli, 
📌Kombe la Mshindi wa Pili Kamba Wanaume,
📌Kombe la Mshindi wa Pili Kamba Wanawake na
📌Kombe la Mshindi wa Tatu Mpira wa Miguu.

Vilevile timu ya TAKUKURU imepata Medali 10 za Dhahabu katika mbio za Mita 100, Mita 200, Mita 800, Mita 1,500, Mita 3,000 na Mita 100 x 4 (Relay), pamoja na Mchezo wa Mbio za Baiskeli. Medali 23 za Shaba katika Mpira wa Miguu na Medali 30 za Fedha katika Mchezo wa Kuvuta Kamba.

Mashindano ya Michezo ya SHIMIWI yalianza Septemba 1, 2025 na kufikia kilele Septemba 16, 2025 ambapo wanamichezo 63 walishiriki michezo ya Mpira wa Miguu, Kuvutana kwa Kamba Wanaume na Wanawake Riadha pamoja na Michezo ya Jadi.

No comments:

Post a Comment