Timu zaanza vyema michuano ya 39 ya SHIMIWI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 1, 2025

Timu zaanza vyema michuano ya 39 ya SHIMIWI

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Timu za Ofisi ya Rais Ikulu, Mahakama, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Hazina ni  baadhi ya timu zilizoanza vyema kwa kushinda kwenye mechi za mchezo wa netiboli, kamba na mpira wa miguu, katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali Jijini Mwanza.

Timu ya Ofisi ya Rais Ikulu waliwavuta Wizara ya Ujenzi kwa wanaume kwa mivuto 2-0; huku kwa wanawake Mahakama wakiwavuta RAS Kagera kwa mivuto 2-0; na kwa mchezo wa mpira wa miguu timu ya Hazina waliwachapa RAS Morogoro kwa magoli 5-0 na Utumishi waliwaangamiza RAS Morogoro kwa magoli 90-0.

Katika michezo mingine ya netiboli, wenyeji timu ya RAS Mwanza waliwashinda Tume ya Utumishi kwa 50-7; huku Hazina wakiwashinda RAS Shinyanga kwa 28-15; nayo Wizara ya Maliasili na Utalii waliibuka kidedea kwa kuwafunga RAS Lindi kwa 61-5; huku TAMISEMI waliwaliza Tume ya Sheria kwa 22-11; na Ofisi ya Maadili waliwafunga Wizara ya Ardhi kwa 26-24.

Timu zilizopata ushindi wa chee baada ya wapinzani wao kushindwa kutokea uwanja Wizara ya Nishati ilipata ushindi wa chee kwa RAS Singida ; huku Wizara ya Mifugo walipata ushindi wa mezani dhini ya Maendeleo ya Jamii.

Katika michezo wa mpira wa miguu iliyofanyika Bwiru Sekondari timu ya Wizara ya Ujenzi waliwafunga Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa magoli 2-0; huku RAS Lindi waliwashinda ndugu zao wa RAS Tanga kwa magoli 3-0; michezo iliyofanyika uwanja wa Nsumba Seminari timu ya Maadili waliwashinda RAS Pwani kwa 3-0; nao mabingwa watetezi Utumishi wameanza vyema   kwa kuwafunga RAS Mbeya kwa magoli 2-0; katika uwanja wa Mabatini Ofisi ya Waziri Mkuu Sera waliwachakaza Pamba kwa magoli 7-0.

Katika mchezo wa kuvuta kamba kwa wanawake washindi matokeo yakiwa kwenye mabano ni Mahakama waliwaadhibu RAS Kagera (2-0); Wizara ya Katiba na Sheria waliwashinda Hazina (2-0); Wizara ya Madini waliwaliza Wizara ya Uchukuzi (2-0); Wizara ya Afya waliwachapa Wizara ya Ujenzi (2-0); Ofisi ya Mashtaka waliwavuta RAS Shinyanga (2-0); TAMISEMI waliwaadabisha RAS Kilimanjaro (2-0); Tume ya Sheria waliwaliza Uwekezaji (2-0); nayo TAKUKURU waliwafunga Wizara ya Mifugo na Uvuvi (2-0).

Matokeo mengine RAS Tanga waliwavuta Ofisi ya Makamu wa Rais (2-0); Wizara ya Viwanda na Biashara walichapwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera (2-0); huku Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wametoana jasho na Waziri Mkuu Kazi (1-1); wakati timu zilizopata ushindi wa chee baada ya wapinzani wao kutoonekana viwanjani ni pamoja na Wizara ya Mawasiliano baada Wizara ya Maji kuchelewa; huku Mfuko wa Mawasiliano wa Umma (UCSAF) baada ya RAS Pwani kutoonekana; nayo  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipewa ushindi dhidi ya Wizara ya Kilimo na Wizara ya Ardhi walipata ushindi dhidi ya Tume ya Utumishi.

Katika michezo ya wanaume walioshinda ni Mahakama dhidi ya Wizar aya Viwanda (2-0); Wizara ya Mifugo waliwashina Maadili (2-0); Wizara ya Ardhi waliwaliza UCSAF 2-0; Wizara ya Mambo ya Ndani waliwavuta Wizara ya Madini (2-0); Wizara ya Maliasili na Utalii waliwaadabisha Uwekezaji (2-0); huku Hazina waliwaadhibu Wizara ya Elimu (1-0); nazo Mashtaka na Tume ya Sheria zimemaliza kwa 1-1; na Wakili Mkuu dhidi ya wizara ya Mawasiliano kwa 1-1.

Wakati zilizopata ushindi wa chee ni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora baada ya RAS Pwani kutoonekana kiwanjani; huku Tume ya Sheria walipata ushindi dhidi ya Ofisi ya Bunge; na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera walipata ushindi dhidi ya Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Maji walishinda dhidi ya Wizara ya Kilimo ambao nao hawajafika uwanjani.

Michezo hiyo inaendelea kesho Jumanne tarehe 02 Septemba, 2025 kwa michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume. 

No comments:

Post a Comment