WAPIGAKURA WA LINDI MJINI USO KWA USO NA DKT. SAMIA HII LEO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 25, 2025

WAPIGAKURA WA LINDI MJINI USO KWA USO NA DKT. SAMIA HII LEO


Maelfu ya wananchi na Wapigakura wa Lindi Mjini Mkoani Lindi leo Alhamisi Septemba 25, 2025 watapata fursa ya kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwa na Mikutano miwili hii leo Mkoani humo ili kuomba kura na kueleza yale ambayo Chama chake kimepanga kuwafanyia wananchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Dkt. Samia mwenye kaulimbiu ya "Kazi na Utu, tunasonga mbele" Jana Jumatano amekuwa na mikutano kwenye Wilaya za Mtama na Ruangwa Mkoani Lindi, akiahidi mara zote kuongeza bidii katika kushughulikia mahitaji muhimu kwenye sekta za afya, elimu, maji, elimu na umeme, akieleza kuwa shabaha yake ni kukuza uchumi na maendeleo ya Mtanzania pamoja na kuweka mazingira rafiki ya kiuchumi katika kuondokana na umaskini kupitia shughuli za kiuchumi.

Mgombea huyo wa kwanza mwanamke kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi CCM ameahidi pia kukuza fursa za ajira kwa vijana kupitia uwezeshaji mbalimbali ikiwemo kusimamia uendelevu wa mikopo ya asilimia kumi ya Halmashauri kwa Vijana, wanawake na wenye ulemavu, kuendeleza ruzuku za mbolea na pembejeo za kilimo, uanzishwaji wa skimu na mabwawa ya umwagiliaji pamoja na ujenzi wa kongani za Viwanda kila Wilaya nchini ili kutoa fursa za uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo na misitu.

Kwa Lindi Mjini yenye kujumuisha eneo la Mchinga Dkt. Samia kupitia Ilani anayoinadi anatarajjwa kuwaeleza wananchi juu ya dhamira yake ya ujenzi wa vituo vya afya Kitumbikweta, Rutamba, Nangaru, ujenzi wa Zahanati za Namkongo, Mpulwa, Mkwaya na Namtamba, ukarabati wa Kituo cha afya Rutamba pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Wilaya.

Ameahidi pia ujenzi wa barabara ya Mtange- Kinengene Kibaoni (Km 5) kwa kiwango cha lami, ujenzi wa barabara ya Bohari- Ofisi za NIDA (Km. 1.5) kwa kiwango cha lami, ujenzi wa barabara ya Mahakama- Mitwero kwa kiwango cha lami, barabara ya Kikwetu- Kibumbwi kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa barabara zenye mteremko mkali kwa kiwango cha zege katika maeneo ya Lindi Mjini, Muhimbili, Matopeni, Mtanda, Mwenge na Wales.

No comments:

Post a Comment