
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax, tarehe 20 Septemba 2025, alikutana na kufanya Kikao na Viongozi wa Maafisa usafirishaji kwa njia ya Pikipiki (Bodaboda) wakiwawakilisha kundi kubwa la Bodaboda Wilaya Magu mkoani Mwaanza, Kikao ambacho kimetokana na maombi ya mara kwa mara ya Viongozi wa Bodaboda kuomba miadi ya kukukutana na kuzungumza na Waziri Dkt. Tax. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya Magu ndugu Fratha Andrea Katumwa.
Baada ya kusikiliza changamoto za Maafisa usafirishaji hao, Dkt Tax amewapongeza kwa umoja wao na kuahidi kushirikiana na Uongozi wa Wilaya Magu kuzitatua changamoto hizo haraka iwezekanavyo ili kuwapunguzia adha hizo ikiwemo uanzishwaji wa SACOS ya Bodaboda Magu.
Aidha, ametoa wito kwa Viongozi hao kuwahamasisha wafuasi wao kujitokeza kwenda kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba 2025 ili kutumia haki yao ya Kikatiba.
Akihitimisha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, amewataka Bodaboda kote nchini kuwa mabalozi wazuri wa kulinda amani ya Nchi wawapo katika shughuli zao kwakuwa wanakutana na kuwahudumia watu wengi hivyo watumie fursa vilivyo na wajiepushe na vitendo vya uhalifu ili waweze kujiletea maendeleo.

No comments:
Post a Comment