DKT. SAMIA AAHIDI KASI ZAIDI YA KUWATUMIKIA WANANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, September 21, 2025

DKT. SAMIA AAHIDI KASI ZAIDI YA KUWATUMIKIA WANANCHI


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendeleza kasi ya maendeleo wilayani Mbinga kupitia miradi mikubwa ya afya, elimu, maji, kilimo, biashara na miundombinu ya barabara.

Katika sekta ya afya, Serikali ya CCM imekamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbinga, vituo vitano vya afya katika maeneo ya Namswea, Linda, Nyoni, Ukata na Langiro pamoja na zahanati 54 zilizojengwa na kukamilishwa katika tarafa mbalimbali. Aidha, nyumba 30 za watumishi wa afya, maabara ya Kituo cha Afya Linda na miundombinu ya maji safi na taka kwenye vituo vya afya pia imekamilika.

Kwa upande wa barabara, miradi mikubwa ya ujenzi kwa kiwango cha lami na changarawe imeendelea kutekelezwa, ikiwemo barabara ya Kitai – Lituhi (km 84.5), barabara ya Mbinga – Litembo – Mkiri (km 47), pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa na madogo zaidi ya 20 katika maeneo mbalimbali. Hali hii imeboresha usafiri na usafirishaji wa mazao ya kilimo na biashara.

Katika elimu, Serikali imejenga zaidi ya vyumba 200 vya madarasa ya shule za msingi, shule mpya za sekondari, mabweni, maktaba, hosteli na nyumba za walimu, huku ikikamilisha pia majengo ya maabara na madarasa ya awali. Hatua hizi zimesaidia kuongeza fursa za watoto kupata elimu bora.

Kwa upande wa kilimo na biashara, Mbinga imepewa kipaumbele kwa kuendeleza mashamba ya kahawa, kugawa miche 10,000 kwa wakulima, kujenga masoko ya mazao na kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata nafaka. Aidha, miradi ya maji katika maeneo ya Nyoni, Kipololo, Maguu, Kitura na Ntunduwaro imeendelea kuwanufaisha wananchi kwa kuwapatia maji safi na salama.

Dkt. Samia amesisitiza kuwa Serikali ya CCM itaendeleza pia miradi ya uvuvi, misitu, ufugaji nyuki, michezo na ujenzi wa miundombinu ya stendi, masoko na machinjio ya kisasa kwa lengo la kuinua kipato na kuboresha maisha ya wananchi.

No comments:

Post a Comment