
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kiteto tarehe 10 Oktoba, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mh. Boniface LIHAMWIKE imetolewa hukumu katika shauri la jinai Na. 03/2025 Jamhuri dhidi ya Bw. SILOMA MANYINDO MTERO.
Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Oktoba 10, 2025, mshtakiwa ametiwa hatiani kwa makosa ya KUOMBA na KUPOKEA Rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) na 15(2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 marejeo ya 2023.
Mshtakiwa alitenda Makosa hayo kwa kuomba kiasi cha Tzs 600,000/= kwa wakulima wa Kata ya Sunya na kuwapa ahadi ya kuwasogezea mipaka ya Msitu wa SULEDO ili waweze kufanya shughuli za kilimo katika hifadhi hiyo ya Msitu wa SULEDO, kitendo ambacho ni kinyume na sheria na kanuni za hifadhi ya msitu wa SULEDO.
Kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Bw. Abdulrahim Jamal Mockray.
Mahakama imemtia hatiani na kuamuru kulipia faini ya kiasi cha Tzs 500,000/= kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela endapo atashindwa kulipa faini hiyo.
Mtuhumiwa alilipa faini ya Tshs 1,000,000/=
TAKUKURU (W) Kiteto Oktoba 10, 2025.
No comments:
Post a Comment