Na Abdala Sifi - WMJJWM- Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amewataka watumishi wa Wizara hiyo kupendana kuthaminiana, kusaidiana, kushirikiana katika utendaji wa kazi ili kuleta Umoja na kufanikisha ya Serikali ya kuihudumia jamii.
Dkt. Jingu amesema hayo tarehe 10 Oktoba 2025, wakati wa kikao cha Watumishi katika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
"Hakuna mtumishi bora kuliko mwingine, naomba tujenge upendo kuheshimiana, kubaliana na kuthaminiana kwa kuwa sisi wote ni sawa na tunafanya kazi moja" amesema Dkt. Jingu.
Aidha Dkt. Jingu, amesisitiza nidhamu katika kazi na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza azma ya Serikali katika kuhudumia wananchi na kuwawezesha kupata maendeleo na ustawi wao.
Dkt. Jingu ameongeza kuwa kila mtumishi anapaswa kujenga tabia shirikishi katika utendaji wa kazi ili kuleta ufanisi wa kazi.
"Niwaombe watumishi wenzangu tuimarishe ushirikiano miongoni mwa watumishi katika kila idara na vitengo, kila mtumishi akifanya kazi yake vizuri basi Wizara na Serikali itakuwa imefanikiwa kutoa huduma bora kwa jamii" amesema Dkt. Jingu.
Amewahimiza watumishi kuendelea kujielimisha Ili kuongeza ujuzi na maarifa kulingana na mabadiliko ya teknolojia ili kuongeza ufanisi na ubunifu kazini.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Felister Mdemu amesema Watumishi na Viongozi wanatakiwa kuhakikisha wanashirikiana ili kuleta ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu.
Kwa upande wao, baadhi ya watumishi wameishukuru Serikali kwa kuwawekea mazingira mazuri ya utendaji wa majukumu ikiwa ni pamoja na uwepo wa Jengo jipya la Wizara ambalo limeleta chachu katika utekelezaji wa majukumu.

No comments:
Post a Comment