
Waziri wa Maji na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani Mkoani Tanga Mhe. Jumaa Aweso amemtaja Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM kama Kiongozi wa aina yake na wa pekee anayetoa maelekezo, uwezeshaji pamoja na ufuatiliaji wa karibu katika kuhakikisha ahadi, maelekezo na majitaji ya wananchi yanatekelezwa kikamilifu katika dhamira yake ya kukuza, kuheshimisha na kustawisha utu wa Mtanzania katika huduma za Maji safi, salama na ya Uhakika.
Aweso amebainisha hayo leo Jumanne Oktoba 07, 2025 Kwenye Viwanja vya Tabasamu Mjini Sengerema, wakati wa Mkutano wa Mgombea Urais Dkt. Samia Mkoani Mwanza, akisema kutokana na utashi huo wa Dkt. Samia, miradi iliyokuwa imeshindikana tangu mwaka 1970 imewezekana kwenye Uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
Mwanasiasa huyo Kijana aliyeambatana na Dkt. Samia Mkoani Mwanza ameeleza pia kuhusu mafanikio ya usambazaji wa maji Vijijini, akisema wakati Dkt. Samia anaingia madarakani miaka minne iliyopita ni Vijiji 5,000 pekee vilivyokuwa na maji safi na ya uhakika kati ya Vijiji 12, 318, na leo Vijiji 10, 579 vina huduma ya Maji safi na salama, akimuhakikishia Dkt. Samia kuwa kabla ya mwaka 2030 Vijiji vyote vya Tanzania vitakuwa vimefikiwa na huduma ya maji safi na salama.
Waziri huyo wa Maji amebainisha pia jitihada zinazochukuliwa sasa na serikali ya Rais Samia, akisema ipo miradi zaidi ya 1,000 inayotekelezwa kote nchini kwa sasa pamoja na mradi wa Visima 900 unaotekelezwa kupitia mitambo ya uchimbaji visima na utengenezaji wa Mabwawa kwenye Mikoa yote ya Tanzania, akisema kukamilika kwa miradi hiyo kutafanikisha adhma ya Dkt. Samia ya kufikisha huduma ya Maji kwa Kila Mtanzania wa Kijijini na Mijini.
No comments:
Post a Comment