
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Asharose Migiro wakitoa elimu ya Mpigakura kwa wananchi wa Ilala Mkoani Dar Es Salaam leo Jumatano Oktoba 22, 2025 kwenye Viwanja vya Kecha, Kinyerezi Mkoani Dar Es salaam, mara baada ya kuhitimisha hotuba yake na kuomba kura kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Dkt. Samia anaendelea na Mikutano yake ya Kampeni na utoaji elimu hiyo ya namna ya kupiga kura kulingana na kanuni za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi wakati huu ambapo bado siku saba pekee Watanzania washiriki kwenye zoezi la Upigaji kura kwa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais wa Tanzania hapo Oktoba 29, 2025 ili kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo.
No comments:
Post a Comment