UTULIVU WA DKT. SAMIA UMEMTOFAUTISHA NA VIONGOZI WENGINE- MCH. MSIGWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 22, 2025

UTULIVU WA DKT. SAMIA UMEMTOFAUTISHA NA VIONGOZI WENGINE- MCH. MSIGWA



Mchungaji Peter Saimon Msigwa, Mbunge mstaafu na Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema awali Vyama pinzani vilikuwa vikibeza na kuamini kuwa Rais Samia Suluhu Hassan angeshindwa kuendeleza miradi ya Kimkakati zaidi ya 17 aliyoachiwa na Mtangulizi wake, akisema Utulivu na Utu wa Dkt. Samia ambaye sasa ni Mgombea Urais katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 umewezesha kukamilisha miradi hiyo pamoja na mingine mingi aliyoianzisha ndani ya Miaka minne ya Uongozi wake.


Msigwa amebainisha hayo leo Jumatano Oktoba 22, 2025 wakati wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya Kecha, Kinyerezi, Ilala Mkoani Dar Es Salaam, akimpongeza kwa namna ambavyo amefanikiwa katika kuijenga Tanzania yenye ustawi kwa wote pamoja na kuendelea kuwa nchi yenye kuzingatia na kuheshimu utu, haki, usawa na uwepo wa huduma muhimu za Kijamii.


Mwanasiasa huyo wa zamani wa Chadema vilevile ameeleza mafanikio makubwa ya dhamira ya Dkt. Samia ya kuenzi na kuendeleza ndoto za watangulizi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akisema maendeleo makubwa na uwekezaji uliofanywa kwenye sekta ya Kilimo nchini ilikuwa maelekezo na ndoto za Mwalimu Nyerere za kutaka Kilimo kiwe uti wa uchumi na maendeleo.

Amemtaja Dkt. Samia pia kama Kiongozi anayeishi kwa vitendo na kuujua vyema uchumi akisema uwekezaji kwenye sekta ya miundombinu ya usafiri na usafirishaji pamoja na miradi mingine ya maendeleo ni sehemu ya kuendelea kuhakikisha Jiji la Dar Es Salaam linaendelea kuwa Kitovu cha biashara nchini na Pembe ya Afrika Mashariki, akiwasihi wananchi wa Mkoa huo kumpa kura za kishindo katika uchaguzi Mkuu wa Jumatano ijayo, Oktoba 29, 2025.

No comments:

Post a Comment