DKT. SAMIA KUTIKISA KWENYE KAMPENI MKOANI KAGERA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 15, 2025

DKT. SAMIA KUTIKISA KWENYE KAMPENI MKOANI KAGERA


Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatano Oktoba 15, anatarajiwa kuwa na mikutano Mitatu ya Kampeni za uchaguzi Mkuu kwenye Mkoa wa Kagera, akifika Muleba, Kyaka na Kayanga kunadi sera, ilani ya Chama Chake pamoja na kuomba kura za wananchi kuelekea uchaguzi Mkuu.

Dkt. Samia anaanza kampeni zake Mkoani Kagera akitokea Mkoa wa Geita Juzi jumatatu, wananchi wa Mkoa huo wakijitokeza kwa wingi kumlaki na kumshukuru kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo, akiwatoa wasiwasi wananchi kuwa Oktoba 29, 2025 serikali na Vyombo vya dola vimejipanga kikamilifu kuhakikisha amani inatawala na kila mmoja anakuwa na mazingira tulivu na salama ya upigaji kura.

Anaingia Mkoani humo wakati huu ambapo ndani ya miaka minne ya Uongozi wake amefanikisha ujenzi wa Hospitali 2 za Bukoba DC na Manispaa, ongezeko la upatikanaji wa maji safi na salama Bukoba Vijijini kutoka asilimia 76 hadi 83, upanuzi wa bandari ya Bukoba pamoja na kuanzisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi Bukoba na ujenzi wa barabara za njia nne Bukoba Mjini.

Kwa Karagwe Serikali ya awamu ya sita imefanikisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Karagwe, Vituo vya afya na Zahanati, utekelezaji wa mradi wa maji Rwakanjunju utakaohudumia Kata 12, huku Kyerwa wakifanikiwa kujenga Hospitali ya Wilaya, shule ya mchepuo wa Kiingereza Wilayani humo na vyumba vya maduka ya biashara katika Kituo cha mabasi cha Nkwenda.

Aidha kwa Misenyi serikali ya Dkt. Samia imefanikisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, soko la ndizi Rukurungo, wakati kwa Muleba Hospitali ya Wilaya imejengwa, limeanzishwa shamba la kahawa kwaajili ya Vijana kwenye Kijiji cha Makongora (Ekari 400) sambamba na kuendelea na ujenzi wa soko la Kisasa kwenye Wilaya hiyo ya Muleba huku Biharamulo nao wakinufaika na ujenzi wa hospitali ya Wilaya, kuiunganisha Biharamulo na Ngara kwenye Gridi ya Taifa na ujenzi wa barabara ya lami ya Murugarama- Rulenge- Nyakahura yenye urefu jumla wa Kilomita 85.

Kwa Wilaya ya Ngara ndani ya miaka minne ya Dkt. Samia, wananchi pia wamenufaika na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa mradi wa shule ya Amali katika eneo la Kasharazi kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.6, ujenzi wa shule ya mchepuo wa Kiingereza pamoja na ujenzi wa mradi wa maji Kumuyange, soko la Kimkakati Kahaza na kuunganisha Wilaya ya Ngara kwenye Gridi ya umeme ya Taifa mchakato ulioenda sambamba na kuanza kwa ujenzi wa kituo cha kupooza umeme na laini ya kusafirisha umeme wa msongo wa 220 KV kutoka Benaco hadi Kyaka.

No comments:

Post a Comment