Na: Dickson Bisare Okuly Blog - Dar Es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amekabidhi kiasi cha shilingi Milioni kumi na tano kwa timu ya Simba SC ikiwa ni zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kwa timu hiyo, baada ya mchezo wa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) dhidi ya timu ya Nsingizini Hotspurs.
Msigwa amekabidhi fedha hizo Oktoba 23, 2025 jijini Dar es Salaam, ambapo Viongozi wa Simba SC waliishukuru Serikali kwa moyo wa kuthamini michezo na kuahidi kuendelea kufanya vizuri katika hatua zinazofuata za mashindano hayo.
Katika mchezo uliochezwa nchini Eswatini Oktoba 19, 2025 klabu ya simba iliibuka na ushindi wa goli 3-0.
No comments:
Post a Comment