MICHEZO YALETA MSHIKAMANO NA AFYA KWA WATUMISHI MADINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

MICHEZO YALETA MSHIKAMANO NA AFYA KWA WATUMISHI MADINI



Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Wizara ya Madini leo Oktoba 18, 2025, imeshiriki Bonanza la Michezo lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin jijini Dodoma, likiwakutanisha watumishi kutoka taasisi zote za Wizara. Bonanza hilo limekuwa sehemu ya utaratibu wa kila robo mwaka ulioanzishwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, kwa lengo la kujenga mshikamano, afya bora, na kuimarisha ari ya watumishi kuweza kuitumikia Serikali ipasavyo.

Akizungumza katika bonanza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya Samamba amesema michezo ni nguzo muhimu ya kuimarisha umoja, afya za watumishi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ili waweze kuishi maisha marefu na hatimaye kuongeza ufanisi kazini na kutimiza malengo iliyowekewa Wizara na Serikali.

Aidha, amewahimiza watumishi wote kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura ili, kuchagua viongozi bora wenye dira ya kuweza kuisimamia Sekta ya Madini kwa maendeleo ya sekta na maendeleo kwa taifa kwa ujumla kwa kusikiliza sera na kuwahamasisha wengine na hatimaye kuwachagua viongozi wanaofaa.

Pia, amezitaka taasisi zote chini ya wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa tija na matokeo, ili kuiheshimisha Sekta mbele ya watanzania na jumuiya ya kimataifa, kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa ushauri, tafiti na mitambo na kuendelea kuhamasiaha uwekezaji nchini kwa kutoa taarifa za uwazi na uwajibikaji kwa kampuni za madini.

‘’Niendelee kuwapongeza sana taasisi zote, Tume ya madini kuendelea kutuheshimisha kwenye makusanyo, STAMICO kuendelea kuwaelea wachimbaji wadogo, kuwapata ushauri na mitambo na kuwa nao karibu, GST kuendelea kuwasaidia wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo kwenye masuala ya kijiolojia, TEITI kuendelea kutoa taarifa kwa uwazi kwenye sekta ya Madini ili wananchi wafahamu mwelekeo na imechangia kitu gani na kikubwa zaidi kuwavutia wawekezaji kuhusu wazi na usimamizi wa rasilimali madini,’’ amesema Eng. Samamba.

Bonanza hilo limehusisha taasisi zifuatazo; Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI)

Aidha, limehusisha jogging ya pamoja, michezo ya mbio za mita 100 kwa wanaume na wanawake, mpira wa miguu ambapo timu ya Tume ya Madini na STAMICO zimeifunga timu ya Wizara na GST kwa magoli 4-1, mpira wapete kwa timu ya GST na TEITI zimeishinda timu ya Wizara na STAMICO kwa vikapu 17-14, mchezo wa kamba wanawake imeshinda timu ya Wizara .

Michezo mengine imehusisha kukimbia na mayai kwa wanawake na wanaume na mpira wa kikapu. Katika michezo hiyo, Eng. Samamba ametoa medali na makombe kwa timu zilizoshinda pamoja na mshindi mmoja mmoja. Aidha, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo ametoa kikombe maalum kwa mchezaji bora Eng. Samamba ikiwa ni maalum kutokana na kuhamasisha michezo kwa watumishi wa wizara na taasisi kushiriki katika michezo.

Akizungumza Dkt. Lekashingo amesema,’’ tunakushuru Katibu Mkuu kwa kuendelea kuhamasisha michezo miongoni mwa watumishi wawizara, na hili linatupa ushindi katika nyanja zote.

"Ndugu mgeni rasmi tumeanza bonaza hili saa 12 asubuhi kwa Jogging ya pamoja ikiwa ni ishara ya kuamsha miili na kuongeza ari ya michezo,’’ amesema Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bi. Beatrice Matemu.






No comments:

Post a Comment