Umati Mkubwa wa wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kibaoni, Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya shule ya msingi Kakuni, ikiwa ni Mkutano wake wa pili na wa mwisho Mkoani humo leo Jumamosi Oktoba 18, 2025.
Katika salamu zake Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Katavi Ndugu Mussa Kimanta ameahidi ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia, akisema wingi wa wananchi waliojitokeza kwenye Mikutano miwili ya Kampeni ikiwemo Mkutano wa awali wa Mpanda Mjini ni dhihirisho la imani na mapenzi makubwa kwa Dkt. Samia na Chama Cha Mapinduzi kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
No comments:
Post a Comment