DKT. SAMIA AAHIDI KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WALIOPISHA UJENZI WA BARABARA ZA MPANDA, KATAVI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 18, 2025

DKT. SAMIA AAHIDI KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WALIOPISHA UJENZI WA BARABARA ZA MPANDA, KATAVI



Mgombea wa nafasi ya Urais wa Janhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuilekeza Wizara ya Ujenzi kwenda Mpanda Mkoani Katavi, kufanya uhakiki wa madia ya fidia kwa wananchi 1073 waliopisha utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara katika Wilaya hiyo.

Akizungumza na wananchi wa Mpanda na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Mkutano wa Kampeni zake kwenye Viwanja vya Azimio, Mjini Mpanda leo Oktoba 18, 2025, Dkt. Samia licha ya kueleza kuwa madai hayo mengine ni ya muda mrefu, mara baada ya uhakiki kufanyika na kuthibitisha uhalali wa madai hayo, wananchi wote watalipwa kwa kadri ya stahiki zao, mara baada ya kupewa ridhaa ya kuunda serikali.

"Ninazo taarifa za uwepo wa madai ya fidia kwa wananchi waliopisha miradi ya maendeleo. Wapo wananchi 243 wanaodai fidia baada ya kupisha ujenzi wa barabara ya Mpanda- Vikonge iliyokamilika mwaka 2021 na wapo wananchi 830 waliopisha ujenzi wa barabara ya Mpanda- Sitalike mwaka 2012/13 niwaahidi tukithibitisha masai haya niwahakikishie mtalipwa." Amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia katika hatua nyingine amesema sekta ya usafiri Mkoa wa Katavi imeimarika sana ndani ya Kipindi cha miaka minne baasa ya maboresho katika uwanja wa ndege Mpanda ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Jengo la abiria, suala lililoimairisha safari za Mpanda kwenda Dar Es Salaam na hivyo kufungua zaidi na kuimarisha shughuli za biashara Mkoani humo.

Ameeleza pia kuhusu uimarishaji wa mawasiliano kwenye Mkoa huo, akisema serikali yake imekamilisha ujenzi wa minara 63 ya mawasiliano Mkoani humo kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote, akiahidi kuendelea kuimarisha huduma hiyo zaidi Mkoani humo katika Vijiji vichache vya Wilaya ya Tanganyika.

Kwa upande wa Elimu Dkt. Samia ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita pia imetekeleza ujenzi wa miundombinu ya msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa shule maalumu ya wavulana, shule ya sayansi ya wasichana, ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu cha kilimo Sokoine, akisema lengo la Chama chake ni kuhakikisha kila mtoto anapata fursa ya elimu kuanzia ile ya awali mpaka chuo kikuu bila ya kujali hali ya uchumi wa Kaya yake.


No comments:

Post a Comment