Na OKULY JULIUS, OKULY BLOG , DODOMA
Serikali imetangaza jumla ya nafasi 41,500 za ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kuwataka Watanzania wenye sifa stahiki kuchangamkia fursa hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumamosi Oktoba 11, 2025, katika Ofisi za Utumishi zilizopo Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi, amesema ajira hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa serikali wa kupunguza upungufu wa watumishi katika sekta mbalimbali za umma.
Kwa mujibu wa Mkomi, ajira hizo zinagawanyika katika kada zifuatazo: elimu (12,176), afya ngazi ya serikali za mitaa (10,280), kilimo (470), mifugo (312), uvuvi (47), na ulinzi unaohusisha Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji (7,000), pamoja na kada nyingine mbalimbali.
Aidha, Mkomi ameielekeza Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kukamilisha mchakato wa ajira zote ambazo hazijajazwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo jumla ya ajira 45,000 zilitengewa, sambamba na ajira mpya za mwaka 2025/2026, ifikapo Novemba 2025.
“Hadi kufikia Novemba mwaka huu, tunataka vibali vyote vya ajira 86,500 vilivyotolewa kwa mwaka 2024/2025 na 2025/2026 viwe vimejazwa, na waliopata ajira hizo waanze kazi mara moja ili kuziba upungufu wa watumishi uliopo nchini,” alisema Mkomi.
Katibu Mkuu huyo pia ameagiza barua za ajira za watumishi wapya zitolewe kupitia akaunti zao za Ajira Portal, badala ya kufika Dodoma, ili kupunguza usumbufu na gharama kwa waombaji.
“Usaili wa wanaoomba ajira serikalini utafanyika katika mikoa husika, na barua za ajira zitawasilishwa kupitia akaunti za portal. Hatutaki waombaji waje Dodoma kwa ajili ya kukusanya barua, kisha warudi tena kwenye vituo vyao,” alisisitiza.
Ameongeza kuwa, kwa sasa serikali ina upungufu wa watumishi wa umma takriban 280,000, na juhudi zinaendelea kuhakikisha pengo hilo linazibwa kwa kutoa vibali vya ajira katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.
Katika hatua nyingine, Mkomi ametoa taarifa ya tathmini ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa watumishi wa umma, ambapo jumla ya watumishi 312 walihudumiwa. Amesema changamoto kubwa zilizojitokeza ni matumizi ya mifumo ya PEPMIS na PIPMIS, ambapo watumishi walipatiwa msaada wa kitaalamu ili kuongeza ufanisi katika matumizi ya mifumo hiyo.

No comments:
Post a Comment