NCHI ZA AFRIKA ZAJADILI KUKUZA MAPATO YA NDANI KUEPUKA UTEGEMEZI WA MISAADA NA MIKOPO KUTOKA NJE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 15, 2025

NCHI ZA AFRIKA ZAJADILI KUKUZA MAPATO YA NDANI KUEPUKA UTEGEMEZI WA MISAADA NA MIKOPO KUTOKA NJE


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, wakifuatilia jambo wakati wa Mkutano wa 52 wa Kundi la Kwanza la nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency Policy Dialogue), uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Nchi 14 za Afrika za Sub-Sahara za Kundi la Kwanza ambazo ni wanachama wa Shirika hilo zilikubaliana kuimarisha mikakati ya kukuza uwekezaji kutoka sekta binafsi na kuimarifa mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani katika nchi zao ili kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa fursa za mikopo na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, wakiteta jambo wakati wa Mkutano wa 52 wa Kundi la Kwanza la nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency Policy Dialogue), uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Nchi 14 za Afrika za Sub-Sahara za Kundi la Kwanza ambazo ni wanachama wa Shirika hilo zilikubaliana kuimarisha mikakati ya kukuza uwekezaji kutoka sekta binafsi na kuimarifa mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani katika nchi zao ili kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa fursa za mikopo na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) na Waziri wa Fedha na Maendeleo wa Lesotho, Dkt. Retselisitsoe Adelaide Matlanyane (Mb) baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 52 wa Kundi la Kwanza la nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency Policy Dialogue), uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Nchi 14 za Afrika za Sub-Sahara za Kundi la Kwanza ambazo ni wanachama wa Shirika hilo zilikubaliana kuimarisha mikakati ya kukuza uwekezaji kutoka sekta binafsi na kuimarifa mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani katika nchi zao ili kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa fursa za mikopo na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.

( Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani)


Na Benny Mwaipaja, Washington D.C


Nchi 14 za Afrika za Sub-Sahara za Kundi la Kwanza ambazo ni wanachama wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), zimekubaliana kuimarisha mikakati ya kukuza uwekezaji kutoka sekta binafsi na kuimarifa mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani katika nchi zao ili kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa fursa za mikopo na misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Hayo yameelezwa wakati wa Mkutano wa 52 wa Kundi la Kwanza la nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency Policy Dialogue), uliofanyika pembezoni mwa Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Akizungumza wakati na baada ya Mkutano huo, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka 2025 ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, alibainisha kuwa makubaliano hayo yamelenga kuimarisha upatikanaji wa rasilimali fedha zitakazosaidia kukuza uchumi na maendeleo ya wananchi.

Alisema kuwa katika Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Afrika, Bw. Adran Ubisse, inaonesha kuwa Tanzania inafanya vizuri katika Mikakati yake ya kuimarisha uwazi wa matumizi ya Bajeti na ujenzi wa mifumo ya kuimarisha ukusanyaji wa fedha za ndani hatua itakayosaidia kupunguza utegemezi wa mikopo na misaada kutoka nje.

Dkt. Mwamba alisema kuwa Tanzania, imeweza kudumisha uthabiti wa uchumi mpana na mwenendo endelevu wa deni la taifa kupitia usimamizi makini wa fedha za umma, unaoongozwa na uratibu thabiti wa sera za kifedha na kiuchumi.

"Katika kipindi cha muda wa kati, tunaendelea kutekeleza sera za ujumlishaji wa fedha za umma (fiscal consolidation) kwa msisitizo wa hatua zinazochochea ukuaji jumuishi, ambazo zimejumuishwa katika programu zetu na Shirika la Fedha Duniani (IMF). Mkakati huu umejengwa katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kama ilivyoainishwa kwenye Mkakati wa Kati wa Mapato (Medium-Term Revenue Strategy), sambamba na ubunifu na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma" alisema Dkt. Mwamba.

Alisema kuwa miongoni mwa mageuzi muhimu yanayotekelezwa ni kuongeza wigo wa kodi kupitia njia za kidigitali za mifumo ya kodi, kuboresha ulipaji kodi kwa hiari, na kuimarisha vyanzo vya mapato vya serikali za mitaa ili kukuza ugatuaji wa fedha.

"Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa hatua za mageuzi ya kifedha zinapangwa kwa umakini, kuepuka kudhoofisha kasi ya urejeshaji wa uchumi, na kulinda matumizi katika miradi ya kijamii na yenye kuhimili athari za tabianchi" Aliongeza Dkt. Mwamba

Kuhusu njia ya kusonga mbele kama Ukanda, alisema kuwa mipango inayoungwa mkono na IMF inapaswa kuendelea kuwa kichocheo muhimu cha kuhamasisha upatikanaji wa fedha zenye masharti nafuu na zenye kuwezesha nchi za Afrika kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, nchi wanachama wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), unahusisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 14 ambazo ni Angola, Tanzania, Botswana, Comoro, Eswatini, Lesotho, Mdagascar, Malawi. Mauritius, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia na zimbabwe.

No comments:

Post a Comment