Maelfu ya wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 19, 2025 kwenye Mkutano wa kampeni Sumbawanga Mjini Mkoani Rukwa kwenye Viwanja vya Kizwite maarufu kama Shule ya Msingi Ndua.
Ikiwa bado siku 10 pekee kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania hapo Oktoba 29, 2025, Dkt. Samia anatumia mikutano hiyo ya kampeni kunadi Ilani ya Chama chake, kuomba kura za ushindi na kueleza makubwa yaliyofanyika kwa miaka yake minne madarakani, akiiongoza serikali ya awamu ya sita.
No comments:
Post a Comment