TARURA YAONDOA VIKWAZO KATIKA BARABARA WILAYANI BAGAMOYO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 11, 2025

TARURA YAONDOA VIKWAZO KATIKA BARABARA WILAYANI BAGAMOYO



Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo, Pwani


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE programu ya uondoaji vikwazo katika barabara (bottleneck) imekalimisha ujenzi wa barabara ya Mtoni-Milo yenye urefu wa Kilomita 5.3 katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Akifafanua juu ya utekelezaji wa mradi huo, Msimamizi wa mradi huo katika wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Bernard Mwita ameeleza kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwa wananchi hasa katika shughuli za kilimo ambazo zilisuasua kutokana na barabara kutopitika.

" Eneo hili lilikuwa halipitiki hivyo kumalilika kwa mradi huu ni ukombozi tosha kwa wananchi hususani katika shughuli za kilimo".

Aidha, ameeleza kuwa moja ya kazi katika mradi huo ilikuwa ni kujenga daraja la midomo mitatu katika eneo lililokuwa korofi ambapo wananchi walilazimika kuvuka kwa kutumia mtumbwi.

Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Geza Ulole, Bw. Joseph Saidi ameipongeza TARURA kwa kukamilisha utekelezaji wa mradi huo ambao kwao nikichocheo kikubwa cha uchumi.

Mradi wa RISE sehemu ya uondoaji vikwazo katika Barabara umetekelezwa kwa awamu ya kwanza katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa mradi huo, sehemu ya pili ya utekelezaji itaendelea kwa lengo la kuondoa vikwazo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ili wananchi waweze kuzifikia huduma za kijamii.

No comments:

Post a Comment