Na Mwandishi Wetu, Chunya
Sekta ya Madini nchini Tanzania inaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na sasa inajulikana kama Sekta jumuishi inayotoa nafasi sawa kwa wote, wanaume, wanawake na vijana kushiriki kikamilifu. Wanawake Wilayani Chunya ni ushahidi wa mabadiliko haya, wakivunja dhana ya zamani kuwa madini ni kazi ya wanaume pekee.
Wakizungumza na Madini Diary hivi karibuni, baadhi ya wanawake hao wameeleza jinsi wanavyoshiriki katika kila hatua ya mnyororo wa madini: wapo wanaomiliki leseni za uchimbaji mdogo, wachimbaji mahiri, wapondaji wa mawe na wafanyabiashara. Wanasema shughuli hizo zimewawezesha kupata kipato, kulea familia, kuanzisha miradi ya maendeleo na kujenga makazi bora.Ushuhuda wao unaonesha wazi kuwa sekta ya madini inayoendeshwa kwa usawa wa kijinsia inaweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wachimbaji Wanawake Itumbi-Chunya Happiness Mabula anasema “Mimi kwenda chini umbali wa mita 200 kuchimba madini ni kitu cha kawaida sana kwangu na nimefanya kazi hii si chini ya miaka 10, nina migodi yangu na nimekua nikilipa kodi kwa Serikali kwa miaka yote na tunawasaidia vijana.
Anaongeza kwamba, kama wanawake wananufaika na shughuli za madini na hivyo kuisaidia jamii. Licha ya mafanikio hayo anasema changamoto zipo kama kuvamiwa maeneo yao.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho Angela Sompo anasema, ‘’kikundi chetu kilianza mwaka 2023 tukiwa wanawake 25, tulianza kwa kuwezeshana kwa kuchangiana vifaa kazi kama makarasha, compressor na mpaka sasa tumekwisha kutoa vifaa kwa wanachama 11 na vifaa hivi vimeturahisishia kazi zetu,’’ na anaongeza, ‘’tulianza kwa kuchangishana michango ya shilingi milioni 1 kila mwezi fedha zilizotusaidia kupata mitaji na kununua vifaa.
Mbali na hayo, Angela anasema amekuwepo kwenye shughuli hizo kwa miaka 10 sasa, anachimba kwenye leseni za mume wake ambazo umempatia mafanikio ya kiuchumi. Angela anasifu juhudi za Serikali kusimamia bei ya dhahabu na sasa wananufaika zaidi.
Kwa upande wa Kikundi cha Wachimbaji wanawake kijiji cha Itumbi iliyopo kata ya Matundasi-Chunya chenye makundi matatu ndani yake ya Wema , Mafanikio na Malkia, Makamu Mwenyekiti wa kikundi Anna Francis anaishukuru Serikali kwa kuwapatia mashine ya kusaga mawe ambayo wameifanya kama chanzo cha mapato kwani inakisaidia kikundi cha kusaga mawe ya kototo kwa ajili ya shughuli za ujenzi. ‘’Tunauza kokoto gari moja la tani 10 kwa shilingi 300,000/ pesa hizo zinaingia kwenye mfuko wetu,". Mbali na vifaa, anaishukuru Serikali kupitia Chama Cha Wanawake Tanzania (TAWOMA) kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika mikutano na makongamano hivyo kupata fursa ya kujifunza zaidi.
Ushiriki wake kwenye shughuli za madini umemuwezesha kusomesha watoto, kujenga nyumba na kuishi vizuri anasema Mariam Hussein mmoja wa wanachama wa kikundi hicho na kuongeza," kuongezeka kwa bei ya dhahabu kumetusaidia sana, kwa gram moja sasa tunapata shilingi hadi Laki mbili na sitini na kusema sasa uchimbaji umebadilika na Chunya imebadilika,".
Vikundi hivyo vitatu tayari vimekwishapatiwa leseni moja ya uchimbaji mdogo iliyopo eneo la itumbi-Chunya bado ingawa bado hawajaanza kuchimba.
Samwel Jeremiah Mhasibu wa Chama Cha Wachimbaji Wadogo Wilaya ya Chunya anasema‘’ Tunamshukuru Rais Samia kwa kuwainua wanawake, lakini Serikali kwa kuanzisha masoko ya madini ya dhahabu kwasababu yanawainua wachimbaji wakiwemo wanawake,". Anaiomba Serikali iwasadie wanawake kupata vifaa vya kuchimba.
"Kutokana na ushiriki wa wa kina mama kwenye shughuli za madini, wameyaona mabadiliko ya wazi Chunya."Sekta ya madini imebadilisha sana Chunya. Chunya sasa ina majengo mazuri, kuna wawekezaji wa kila aina, wa nyumba za biashara, makazi, kampuni za ulinzi, usambazaji wa vifaa. Chunya hii haikuwa hivi kabla,’’ anasema Sofia Mwanauta mwanamke mchimbaji wa madini Chunya na mmoja wa wanakikundi cha Wanawake wachimbaji Chunya .
Serikali itoe upendeleo kwa wanawake kwa kuwapatia leseni za kuchimba zenye madini zilizofanyiwa tafiti ili wachimbe pasipo kubahatisha; wapatiwe elimu kuhusu mfumo wa kuomba leseni na malipo yanayotolewa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwawezesha kwa vifaa vya uchimbaji ili wasitumie nguvu kubwa kwenye shughuli za uchimbaji na kwa taasisi za fedha wameiomba Serikali iendelee kuzungumza na taasisi hizo ili ziweze kulegeza masharti ya kukopa kwa Sekta ya Madini.
Vikundi hivi vimeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia kuweza kufanya kazi zao za uchimbaji kwa uhuru, amani na utulivu. Pia, Serikali kwa kusimamia bei ya dhahabu na kutokuwaacha nyuma wanawake. Aidha, wametoa shukrani kwa Serikali kuwapatia karasha pamoja na kuishukuru kwa kuwahamasisha kujiunga katika vikundi. Vilevile, wamepongeza kwa kuanzishwa masoko ya madini na uwepo wa bei elekezi kwa kuwa yamerahisisha biashara ya madini. Pia, wanawake Chunya wameipongeza Ofisi Madini Chunya kwa kuwasilikiza wachimbaji na kutoa ushirikiano mzuri bila ubaguzi.
Kutokana na manufaa wanayoyapata, wamewaasa wanawake wengine nchini kutokuogopa kushiriki katika shughuli za madini. Wametoa hamasa kwa wanawake kujiunga kwenye vikundi ili kufikiwa na huduma kwa ajili urahisi licha ya kuwepo mtazamo hasi kwa baadhi ya watu juu ya ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya madini, wanawake wachimbaji wanatoa hamasa kwa wengine ya kutokuogopa kwani wanaweza.

No comments:
Post a Comment