
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha, amepokea tuzo maalum kama kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza na kuendeleza mchezo wa kriketi nchini Tanzania.
Tuzo hiyo amekabiziwa na Bw. Hamza R. Pardesi, Mkurugenzi Mtendaji wa NIDA Textiles, katika hafla ya kufunga mashindano ya NIDA TEXTILES CUP yaliyofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yalishirikisha Timu ya Taifa ya wanawake ya Kriketi ya Tanzania na Timu ya Taifa ya wanawake ya Kriketi ya Canada, yakiwa na lengo la kuimarisha uhusiano wa michezo na kukuza ushindani wa kimataifa katika mchezo huo.



No comments:
Post a Comment